Plot for sale at Maendeleo, Mbeya


JE WAJUA?🥸
.
Kuwekeza Kwenye Ardhi (Land Banking) kama Njia Mbadala ya Akaunti ya Akiba Benki
> "Badala ya kuweka pesa kwenye akaunti ya akiba benki kwa muda mrefu, wekeza kwenye ardhi."
âś… Land Banking ni nini?
Ni utaratibu wa kununua ardhi isiyoendelezwa kama uwekezaji, bila mpango wa haraka wa kuijenga.
Wakati mwingine hutumika na kampuni au mtu binafsi anayenunua ardhi kwa madhumuni ya kuijenga baadae.
🔄 Tofauti na Akiba Benki
Akiba benki huathirika na mfumuko wa bei (inflation) – thamani ya pesa hupungua kadri muda unavyopita.
Land banking ni uwekezaji tulivu (passive investment) wa hatari ndogo unaofaa kufikiriwa.
👤 Ni nani anafaa kuzingatia Land Banking?
▪︎Watu wenye biashara nzuri au ajira za uhakika.
▪︎Wale walio na akiba ya pesa isiyopangiwa matumizi ya haraka.
▪︎Watu wasiokuwa na muda wa kuendesha biashara au wasiopendelea hatari kubwa za kuanzisha miradi.
📍 Mfano Halisi
Rafiki yangu alinunua kiwanja chenye hati miliki Arusha–Ngaramtoni Kwa Iddi kwa Tsh. 15M mwaka 2018.
Alitaka kujenga, lakini changamoto zikatokea na akalazimika kuelekeza nguvu zake kwenye biashara.
Hadi sasa, kiwanja hicho kinauzwa kwa zaidi ya Tsh. 45M, bila hata maendeleo yoyote kufanyika!
Kama angekuwa alinunua ekari kwa Tsh.72M, leo angeweza kuuza kwa Tsh. 320M+.
đź§ Jambo la Kukumbuka
Hauhitaji kuwa na kampuni ili uwekeze kwenye land banking.
Unaweza kuwekeza kama mtu binafsi au kama kikundi.
Wakati unapanga cha kufanya, wekeza kwenye ardhi ili utakapofikia uamuzi fedha zako ziwe zimekuwa mara 3 hadi 10 kutegemeana na kasi ya kuongezeka thamani maeneo utakayowekeza.
🙏🏿