Farm for sale at Amani, Muheza, Tanga







#English I am renting a partially developed area for the use of a tourist camp (campsite) with guest houses (unfinished), a dining and meeting hall, a camping site, fire pits and barbecues, and a car parking area, as well as native trees and plants of native cooking spices, including cardamom, cinnamon, and cloves. This campsite is located in Amani, Muheza district, in the Tanga region and is adjacent to the headquarters of the Amani Nature Forest Reserve under the Tanzania Forest Services (TFS) Agency. The campsite borders the Amani Nature Forest Reserve, which is famous for tourism and research activities, especially for birds, lizards, three-horned chameleons, and extinct snakes, apart from the oldest African botanical garden and native flowers like African violets (Saintpaulia), waterfalls, mountaineering, and marathons on foot, bike, and motorbike. #Kiswahili Ninakodisha eneo lililoendelezwa kiasi kwa ajili ya matumizi ya kambi ya utalii (campsite) likiwa na nyumba za wageni (hazijakamilika), ukumbi wa chakula na mikutano, eneo lenye ukoka wa kuweka kambi/mahema (camping site), sehemu za kuota moto na kuchomea nyama, eneo la maegesho ya magari pamoja na miti ya asili na mimea ya viungo vya asili vya kupikia ikiwemo iliki, midalasini, na karafuu. Campsite hii ipo eneo la Amani, Wilaya ya Muheza mkoani Tanga, na liko jirani na Ofisi za makao makuu ya Msitu wa Hifadhi Asilia wa Amani (Amani Nature Forest Reserve) ulio chini ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (Tanzania Forest Services (TFS) Agency). Campsite inapakana kabisa na Msitu wa Hifadhi Asilia wa Amani, ambao ni maarufu kwa shughuli za utalii na utafiti, haswa wa ndege, mijusi, vinyonga wenye pembe tatu, na nyoka wa ajabu mbali na bustani ya zamani ya mimea barani Afrika pamoja na maua ya asili kama African violet (Saintpaulia), maporomoko ya maji, upandaji milima na marathoni za miguu, baiskeli na pikipiki.